FILAMU YA 'MIMI SIYO MWEHU' KUTIKISA ZAIDI YA 'LAANA YA MKE'


Unaikumbuka ile Filamu ya Laana ya Mke iliyoigizwa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga ambayo hivi karibuni ilifanikiwa kushinda Tuzo ya Heshima Filamu Bora yenye maudhui ya kitaifa Kanda ya Ziwa???.

Sasa ni hivi?!! Baada ya Filamu ya Laana ya Mke kutikisa....Wasanii wa Filamu mkoa wa Shinyanga wanakuletea filamu nyingine kali imepewa jina la " MIMI SIYO MWEHU".... Ndiyo!!  Mimi siyo Mwehu ni bonge la filamu yenye tungo zenye manufaa katika jamii zenye kuelimisha, kuonya,kuburudisha zilizojaa mafunzo ya uhalisia wa maisha halisi katika jamii za Kiafrika.

Mwandaaji wa Filamu hiyo, Ibrahim Juma Songoro maarufu 'Songoro Gadafi' ambaye ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga ameiambia Malunde1 blog kuwa filamu ya 'Mimi Siyo Mwehu' inalenga kuelimisha jamii inayowachukulia watu wasio na kipato,waliochoka kimaisha, kiuchumi na kiafya mawazo yao au ushauri wao haustahili bali ni wendawazimu.

"Tumemaliza kutengeneza filamu ya Mimi siyo mwehu...Mimi Sio Mwehu ni filamu iliyosheheni misemo ya hekima itakayomfanya mtazamaji asichoke kuitazama katika maisha yake, washiriki wakuu kwenye filamu hii iliyoongozwa na Director Dave Skerah ni Juma Ibrahim Songoro, Goodness Mndeme na Fadhili Mungi".

"Naapa kurudisha heshima ya tasnia ya Filamu Tanzania kwa kuwaletea Filamu zenye tungo zenye manufaa katika jamii kwa lengo la kuelimisha, kuonya na kuburudisha kwa kuangalia uhalisia wa maisha ya jamii zetu za Kiafrika",amesema Songoro.

Amesema Filamu ya 'Mimi Siyo Mwehu' itazinduliwa hivi karibuni na kuwaomba mashabiki wa filamu kujiandaa kupokea Filmu hii yenye ubora wa hali ya juu.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Songoro

Goodness 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527