IDDY MOBBY WA MWADUI FC ATUA POLISI TANZANIA

Timu ya Polisi Tanzania wameingia Kandarasi ya Mwaka mmoja leo na Beki Kiraka Iddy Mobby Mfaume ambaye msimu uliopita alikuwa anakipiga na wachimba madini ya Almasi Mwadui FC. 

Timu ya Polisi Tanzania inazidi kujiimalisha kuelekea kuanza kwa ligi kuu soka Tanzania Bara katika Msimu wa Mwaka 2019/2020 baada ya kunasa Nyota kadhaa. 

Wafunga Buti hao ambao wanaonekana wamepania kutoa ushindani katika Soka Nchini Tanzania wameendelea kushusha nyota wenye uwezo. 

Mbali Iddy Mobby Polisi Tanzania wameingia mkataba na Hassan Nassor Maulid ambaye amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Ndanda FC, Hassan ni mahiri sana kwenye kucheza namba nane.
Hassan Nassor Maulid akitia alama ya Dole Gumba katika fomu za Polisi Tanzania.

Iddy Mobby Aliyekuwa Nahodha wa Mwadui FC ya wilayani Kishapu mkoani Shinyanga,Pamoja na Hassan Nassor Maulid wameongezeka katika kikosi cha Vijana hao wa IGP Simon Sirro ambao walipanda daraja msimu uliopita na sasa watakipiga katika ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post