MTOTO WA MIAKA 8 AMUUA MTOTO WA JIRANI WA MWAKA 1 KWA KUMKATA PANGA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 24, 2019

MTOTO WA MIAKA 8 AMUUA MTOTO WA JIRANI WA MWAKA 1 KWA KUMKATA PANGA

  Malunde       Wednesday, July 24, 2019

Polisi mkoa wa Morogoro nchini Tanzania linawashikilia baba na mtoto wake wa miaka nane kwa tuhuma za kumuua mtoto wa jirani yao mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kwa kumkata mapanga kichwani.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita Julai 21, 2019 saa 8 mchana katika kijiji cha Hembeti wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo mwili wa mtoto huyo, Greyson Valentino ulikutwa umefichwa kwenye shamba la watuhumiwa ukiwa na majeraha.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Julai 24, 2019, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amewataja watumiwa ni Said Stephen ambaye ni baba na mwanae wa kike (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Mpapa wilaya ya Mvomero

Kamanda huyo amesema siku ya tukio baba wa marehemu, Simon Shedrack akiwa kanisani alipata taarifa kuwa mtoto wake amepotea na hivyo aliamua kurudi nyumbani kuanza kumtafuta kwa kushirikiana na majirani zake.

Amesema katika harakati za kumtafuta walipita kwenye shamba la mtuhumiwa na kuukuta mwili wa mtoto wake ukiwa na majeraha kichwani.

Kamanda huyo amesema baada baba wa marehemu kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ili kuhoji kwa nini mwili wa mtoto wake umekutwa kwenye shamba hilo ndipo mdogo wa mtuhumiwa (jina linahifadhiwa) alipoeleza alimuona dada yake akimuua mtoto huyo kwa kutumia panga kisha kumuweka shamba.

Mutafungwa amesema baada ya tukio hilo wananchi walimkamata mtoto huyo aliyetajwa kuhusika na mauaji hayo na kumfikisha katika kituo cha polisi Dakawa akiwa na panga alilotumia kufanyia mauaji hayo.
Na Hamida Shariff, Mwananchi 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post