BONDIA AFARIKI KWA KIPIGO AKIZICHAPA NA MPINZANI WAKE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 24, 2019

BONDIA AFARIKI KWA KIPIGO AKIZICHAPA NA MPINZANI WAKE

  Malunde       Wednesday, July 24, 2019

Bondia wa Russia, Maxim Dadashev amefariki baada ya kupata majeraha makubwa.

Dadashev aliyekuwa na umri wa miaka 28, alifariki baada ya kupata kipigo alipokuwa akizichapa na mpinzani Subriel Matias London, England.

Dadashev aliondolewa kwa msaada wa machela akionekana mwenye hali mbaya.

Bondia huyo alivuja damu ndani ya ubongo na licha ya kufanyiwa upasuaji haraka, alifariki dunia.

Taarifa ya Russia ilisema inafanya uchunguzi wa tukio la bondia huyo kama kulikuwa na viashiria vya vurugu vilivyotokea ulingoni.

“Tumesikika kumpoteza bondia mwenye umri mdogo aliyekuwa hodari ulingoni, tunaungana na familia ya Maxim Dadashev,”alisema Katibu Mkuu Umar Kremlev.

Bondia huyo amefariki akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yote 13 aliyocheza enzi ya uhai wake.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post