CHADEMA KUTINGA MAHAKAMANI KUPINGA TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE

Na Amiri kilagalila-Njombe

Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema  mapema wiki ijayo kinategemea kufika mahakamani kupinga utaratibu uliyotumika kumvua ubunge aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Antipas Lissu ambaye yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu baada  kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka jana katika eneo la eria D jijini Dodoma.


Hayo yamesemwa  na mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama hicho  John Mrema  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani Njombe  akiwa ameambatana  viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa chama hicho freeman mbowe  ambaye amefanya mkutano wa ndani mjini humo.

Mrema amesema kuwa chama hicho kinaona kuwa utaratibu huo umekiuka sheria kwa sehemu kubwa kwakuwa utenguzi huo umefanyika wakati  mbunge huyo akiwa katika matibabu na kwamba kuhusu kujaza fomu za maadili na mali amesema asingeweza kujaza kwa kuwa hakuwa ndani ya nchi na asingeweza kusainiwa kwa mujibu wa sheria

 Amesema Agenda nyingine ambazo zinajadiliwa katika ziara hiyo katika kanda ya Nyasa ni pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa,kuwashukuru viongozi na wanachama kwa kazi kubwa waliyofanya wakati  mbowe na viongozi wa chadema wakiwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne pamoja na kutoa ufafanuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo imeonyesha kubadili kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyama nchini.

Nao baadhi ya viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo Rose Mayemba kiongozi wa chadema msingi na Alatanga Nyagawa ambaye ni katibu wa mkoa chama wamesema wameanza kuandikisha wanachama katika daftari la maalumu la A3 kuanzia ngazi ya chini na kwamba watanzania wategemee chama hicho kupata ushindi mkubwa kwa kuwa kimejihimarisha katika utunzaji wa taarifa.

Katika ziara hiyo Mbowe  amekagua ujenzi wa jengo la ofisi za chama iliypo katika mtaa wa hagafilo ilyofikia asilimia 95 katika ujenzi wake


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527