TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNEManchester United inapania kumlipa Paul Pogba, 26, hadi pauni nusu milioni £500,000 kwa wiki licha ya Real Madrid na Juventus kumnyatia kiungo huyo raia wa Ufaransa. (Mail)
Bayern Munich haijawasiliana na winga wa Real Madrid Gareth Bale,29, anasema ajenti wa nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (ESPN)

Kocha wa Derby Frank Lampard anajiandaa kukutana na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kujadiliana kuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Maurizio Sarri. (Sun)

Chelsea wanataka kumpatia Lampard,40, mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja wa Stamford Bridge. (ESPN)

Benfica imepuuzilia mbali tetesi kuwa Atletico Madrid itaipiku Manchester City katika usajili wa mshambuliaji wa Ureno, Joao Felix, 19 kwa kima cha pauni milioni £107 na kuzitaja tetesi hizo kuwa "taarifa feki". (AS)Joao Felix

Chelsea wamekataa dau la pauni milioni £35 kutoka kwa Barcelona na Atletico Madrid la kumnunua mshambuliaji wa miaka 30 Mbrazil Willian. (Sky Sports)

Paris St-Germain wanataka kukamilisha mchakato wa usajili wa mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, baada ya michuano ya Copa America. (AS)

Coutinho pia analengwa na Manchester United lakini huenda asiwasikilize kutokana na heshima alionayo kwa klabu yake ya zamani ya Liverpool. (Sky Sports)

Liverpool wamepewa ishara ya kumnunu mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, wa Barcelona endpo wataweza kulipa pauni milioni 90. (TEAMtalk)

Crystal Palace wamekataa dau la pauni milioni 50 iliotolewa na Manchester United kumnunua beki wake wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 21. (Sky Sports)

United pia wamepoteza matumaini ya kumsajili mlizi wa West HamIssa Diop baada ya dau lao la pauni milioni £40m kukataliwa.

Mkataba huo ulihusisha mmoja wa wachezaji wa United kujiunga na klabu huyo japo haijabainika ni mchezaji yupi. (Telefoot, via Metro)Mlinzi wa West Ham Issa Diop

West Ham wameiambia Eibar kuwa wako tayari kulipa ada ya pauni milioni £13.4 kugharamia uhamisho wa kiungo wa kati wa Uhispania Joan Jordan. (Marca)

Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumsajili upya beki wa kushoto wa PSV Eindhoven Mhispania Angelino - Mwaka mmoja baada ya kumuuza kiungo huyo wa miaka 22. (Sun)

Manchester United wanakaribia kufikia mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 31. (Mirror)Mata alitua Old Trafford Manchester United ikiwa chini ya ukufunzi wa kocha wa zamani David Moyes

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, ameambiwa na kocha wa timu ya taifa yake ya taifa Roberto Martinez kwamba "hana budi kuondoka Manchester United". (Het Laatste Nieuws - in Dutch)

Mshambuliaji wa Chelsea muingereza Martell Taylor-Crossdale,19 anafanyiwa vipimo vya matibabu kabla ya kujiunga na Hoffenheim kwa mkataba wa kudumu. (Sky Sports)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post