MWANAFUNZI CHUO KIKUU CHA KAMPALA TAWI LA TANZANIA (KIU) AFARIKI DUNIA KWA KUCHOMWA VISU NJE YA GETI LA CHUO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, June 18, 2019

MWANAFUNZI CHUO KIKUU CHA KAMPALA TAWI LA TANZANIA (KIU) AFARIKI DUNIA KWA KUCHOMWA VISU NJE YA GETI LA CHUO

  Malunde       Tuesday, June 18, 2019
Mwanafunzi wa stashahada ya maabara kutoka Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU), Anifa Mgaya amefariki dunia  Jumapili usiku baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.
Anifa alikutwa na umauti majira ya saa 2 usiku jirani na geti la kuingia katika chuo hicho kilichopo GongolaMboto jijini Dar es Dar es Salaam alichokuwa akisoma.

Taarifa zinaeleza baada ya kushambuliwa, wanafunzi wenzake walijitokeza ili kumpatia msaada kwa kumkimbiza hospitali lakini hadi wanafika alikuwa tayari umauti umemfika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zuberi Chembela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha vijana waliohusika katika tukio hilo wanasemekana kuwa ni vibaka.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post