JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUFANYA UKAGUZI WA VIFAA VYA KUZIMA MOTO KATIKA MAGARI YOTE NCHINI

SALVATORY NTANDU

Jeshi la zimamoto na Ukoaji limewataka wamiliki wa Magari ya abiria na Mizigo kuyapeleka magari yao katika vituo vya ukaguzi vilivyopo chini ya jeshi hilo ili kufanyiwa ukaguzi wa vifaa vya kuzimia moto pamoja na kupatiwa elimu na matumizi sahihi ili kuepuka madhara yatokanayo na majanga ya moto.

Hayo yamebainishwa jana na Kamisha Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji (CGF) THOBIAS ANDENGENYI wilayani Kahama mkoani shinyanga katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazotekelezwa na jeshi hilo.

Amesema ni budi kwa wamiliki wa Magari  kutii agizo hilo ambalo ni takwa la kisheria  ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria kwani elimu juu ya matumizi ya vifaa vya kuzimia moto ni muhimu sana na hawapaswi kupuuza agizo hilo.

Mbali na hilo Kamishina ANDENGENYI amesema  kwa sasa Jeshi la zimamoto na Uokiaji  linatarajia kuanzisha vilabu vya marafiki wa zimamoto na uokoaji katika shule za msingi na sekondari nchini kwa lengo la kutoa elimu juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo wanayoishi.

Nae mkuu wa wilaya ya Kahama, ANAMRINGI MACHA amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za Msalala, Ushetu na Mji kuhakikisha kabla ya kujenga  majengo  ya umma ni lazima ramani zake ziwe zimehakikiwa na Jeshi la zimamoto na uokoaji ili kupewa ushauri wa kitalaam ambao utasaidia kuondoa madhara yatokanayo na moto katika majengo hayo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527