PIERRE LIQUID KUONGOZANA NA WABUNGE HADI MISRI KUISHANGILIA TAIFA STARS


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema wabunge 48 watakwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  katika Fainali za Mataifa ya Afika (AFCON) zinazofanyika nchini Misri wakiambatana na Peter Mollel maarufu Pierre Konki Liquid.


Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Juni 18, 2019 Ndugai amesema wataambatana na mchekeshaji huyo katika fainali hizo huku akiwataka wabunge zaidi kujiandikisha ili kwenda Misri.

Katika fainali hizo zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19, 2019, Taifa Stars imepangwa kundi moja na Algeria, Senegal na Kenya.

Msafara wa wachezaji 32 wa Taifa Stars uliondoka nchini Juni 7, 2019  kwenda Cairo kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ya fainali hizo na tayari timu hiyo imeshacheza mechi mbili za kirafiki na Misri na Zimbabwe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527