MAHAKAMA YA MAFISADI YAMHUKUMU MNIGERIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 21, 2019

MAHAKAMA YA MAFISADI YAMHUKUMU MNIGERIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA

  Malunde       Friday, June 21, 2019

Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumi Uchumi maarufu kama ‘Mahakama ya Mafisadi’ imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela raia wa Nigeria, Christian Ugbechi baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Pipi 56 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Adhabu hiyo imetolewa leo June 21, 2019 na Jaji Sirillius Matupa baada ya mshitakiwa huyo kutiwa hatiani June 19, 2019 ambapo Jaji alishindwa kutoa adhabu kutokana na mvutano wa kisheria.

Mshtakiwa huyo anadaiwa January 28, mwaka jana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) Wilayani Ilala Mkoani DSM, raia huyo alikamatwa akisafirisha dawa hizo zenye uzito wa gramu 947.57.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post