MADAKTARI WALIOSOMWESHWA NA SERIKALI KUPANGIWA VITUO


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema madakatari wote waliosoma kwa fedha za serikali watapangwa katika vituo vya kazi na serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nanyamba Abdalah Chikota (CCM) ambaye alitaka kujua mpango wa muda mfupi wa serikali wa kupeleka madaktari bingwa katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula (Mtwara).

Ndugulile amesema katika wakati huu wa mpito wakiwa wanasubiri kupeleka madaktari hao Serikalini pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF wamekuwa wakiweka kambi mabalimbali wakiwa na madaktari bingwa ili kutoa huduma za kibingwa.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtwara Mjini, Hawa Ghasia (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kupeleka madaktari bingwa katika hospitali ya Ligula, Ndugulile amesema Wizara imefanya tathimini ya mahitaji ya madaktari bingwa na fani zao katika Hospitali zote za mikoa, Kanda maalum na Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwamba tathmini hiyo itawezesha utekelezaji wa uamuzi wa kuwapanga upya madaktari Bingwa kwa uwiano kulingana na mahitaji ya kila Hospitali hizo.

“Lengo ni kuwa kila Hospitali hizi zinakuwa na madaktari bingwa wa fani nane, fanio hizo ni pamoja na Daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake , Watoto, Magonjwa ya Ndani, Upasuaji, Upasuaji wa mifupa, Daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali “ amesema.

Pia amesema madaktari wengine bingwa wanaohitajika katika Hospitali hizo ni pamoja na Daktari bingwa wa huduma za usingizi na daktari bingwa wa huduma ya Radiolojia.

Kwa mujibu wa Ndugulile amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 Wizara iliwapeleka madaktari bingwa wa fani za upasuaji wa kawaida na upasuaji wa mifupa 125 katika Chuo cha MUHAS na wanatarajia kumaliza masomo yao katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post