AZAM FC WABADILI GIA ANGANI KWA CHIRWA

MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Obrey Chirwa, ataendelea kuitumikia timu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo mwenye spidi na mabavu, amefikia makubaliano na Azam FC na kusaini mkataba mpya leo mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'. 
Chirwa aliyefunga bao muhimu kwa Azam FC msimu uliopita kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Lipuli, tayari ameanza maandalizi ya msimu mpya na kikosi cha timu hiyo jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post