IRAN YATUPIWA LAWAMA BAADA YA WAHOUTHI WA YEMEN KUUSHAMBULIA UWANJA WA NDEGE SAUDIA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 13, 2019

IRAN YATUPIWA LAWAMA BAADA YA WAHOUTHI WA YEMEN KUUSHAMBULIA UWANJA WA NDEGE SAUDIA

  Malunde       Thursday, June 13, 2019

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeapa kujibu vikali shambulizi la kombora lililofanywa jana na wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwenye uwanja wa kiraia wa ndege kusini mwa Saudia na kuwajeruhi watu 23. 

Muungano huo, wa waislamu wa madhehebu ya Suni ambao umekuwa ukipambana na vuguvugu la Kihouthi nchini Yemen linaloungwa mkono na Iran umesema shambulizi hilo la mapema jana lilidhihirisha kuwa Iran inatoa msaada kwa kile ulichokiita kuwa ni ugaidi wa nje ya mipaka. 

Muungano huo ulisema kombora hilo lilipiga ukumbi wanakowasili abiria katika uwanja wa Abha, na kusababisha uharibifu.

 Wahouthi walisema katika vyombo vyao vya habari kuwa walifyatua kombora hilo na kuupiga uwanja wa ndege wa Abha ulioko kusini mwa mpaka wa Yemen unaotumika kwa safari za ndani na za kikanda.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post