BEKI WA KMC AMWAGA WINO YANGA SC

Klabu ya Yanga imetangaza kuinasa saini ya Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally 'Mwarabu'  ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Ally amekuwa mlinzi bora ndani ya Kikosi cha KMC kitu ambacho kilimvutia Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa ndani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani kwani wale wa kigeni wamekamilisha maagizo ya mwalimu kwa asilimia 90.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527