STAND UNITED WATANGAZA NAFASI ZA KAZI


Klabu ya Stand United ya mkoani Shinyanga ambayo msimu ujao itashiriki katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara imetangaza nafasi za kazi kwa Kocha mkuu na Kocha msaidizi, ili kuboresha kikosi chake katika harakati za kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara.

Pia timu hiyo yenye maskani yake katika Viunga vya mji wa  Shinyanga imetangaza kupokea wachezaji waliowahi kucheza ligi kuu Soka Tanzania Bara pamoja na wale ambao watatolewa kwa mkopo kutoka vilabu vya ligi kuu soka Tanzania Bara.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527