Picha : WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA WAKUTANA NA BUNGE LA AFRIKA KUJADILI ELIMU KWA WATOTO WA KIKE



Wanaharakati wa haki za binadamu na viongozi wa asasi za kiraia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamekutana na viongozi wa Bunge la Afrika kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu haki za binadamu hususani haki ya mtoto wa kike kupata elimu.





Kikao hicho kilichofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele kutoka nchini Tanzania kimefanyika leo Jumamosi Mei 11,2019 katika ukumbi wa kawaida wa Bunge la Afrika jijini Johannesburg,Afrika Kusini ambapo pia wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Afrika Kusini wameshiriki. 

Wajumbe wa kikao hicho wamejadili kwa kina kuhusu upatikanaji wa elimu kwa watoto  hususani haki ya elimu kwa watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni na walio nje ya shule (Out of school girls in education systems)

Angalia picha za matukio hapa chini
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akifungua kikao cha Bunge la Afrika na viongozi wa asasi za kiraia,wanaharakati,wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Afrika Kusini leo. Mhe. Masele alisema ni vyema nchi za Afrika zikawa na sheria na sera zinazompa mtoto wa kike haki ya kupata elimu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza wakati wa kikao hicho.



Katibu wa Bunge la Afrika,Yusupha Jobe akizungumzia kuhusu nafasi ya asasi za kiraia kushirikiana na Bunge la Afrika katika kupigania haki za binadamu.

Katibu wa Bunge la Afrika,Yusupha Jobe (kulia) akizungumza.
Washiriki wa kikao hicho wakiwa ukumbini.
Wa kwanza kushoto mbele ni Afisa Uraghibishaji kutoka shirika la Under The Same Sun (UTSS) nchini Tanzania linalojihusisha na masuala ya watu wenye Ualbino Perpetua Senkoro akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu na Biashara nchini Tanzania (wa tatu kutoka kushoto),Flaviana Charles wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kinaendelea.

Kikao kikiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527