WATU WENYE SILAHA WASHAMBULIA HOTELI YA KIFAHARI


Wanaume wapatao watatu wenye silaha wamevaimia hoteli ya kifahari huko Gwadar katika jimbo la Balochistan na kuua mtu mmoja, utawala wa nchi hiyo umeeleza.


Vikosi vya usalama vimelizunguka eneo la hoteli hiyo ya ' Pearl Continental'katika mji wa Gwadar baada ya shambulio lililofanywa na watu watatu wenye silaha. Gazeti la Dawm limeripoti.

Milio ya risasi ilisikika kutokea ndani ya hoteli.

Ripoti kamili inayoeleza idadi ya wageni waliokolewa bado haijatoka ingawa tayari wageni wengi waokolewa.
Mji huo ambao ni kituo cha mabilionea wa uwekezaji wa miradi kutoka China.

Na mashambulio ya aina huwa yanawalenga wageni haswa kupinga miradi ya wawekezaji kutoka China.
Aidha hoteli hiyo inatajwa kuwa na wageni wengi kutoka nje ya nchi ambao ni watalii na wafanyabiashara, lakini bado haijajulikana ni wangapi walikuwa katika hoteli hiyo.

Washambuliaji hao walilivamia jengo hilo ambalo ni maarufu kwa wageni kutoka nje , majira ya saa kumi na mbili jioni na kuua askari mmoja aliyekuwa getini.

Shambulio hili lmekuja wiki chache baada ya watu wenye silaha kuua watu 14 na miongoni mwao wakiwa askari katika eneo hilo.

Mashambulio ya aina hiyo ni mengi katika jimbo la Balochistan, eneo ambalo ni la watu maskini zaidi katika nchi hiyo ya Pakistani.

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post