MC PILIPILI KIZIMBANI KWA MAKOSA YA MTANDAO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 7, 2019

MC PILIPILI KIZIMBANI KWA MAKOSA YA MTANDAO

  Malunde       Tuesday, May 7, 2019

Mshereheshaji, Emanuel Mathias (34) maarufu kama MC Pili Pili na mwenzake wameachiwa kwa dhamana katika kesi ya kuchapisha maudhui katika mtandao bila kuwa na leseni ya  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA).

Mbali na Mathias, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Heriel Clemence( 25) ambapo wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.


Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai wakati akisoma hati ya mashtaka leo Mei 7, 2019, kuwa wawili hao walitenda kosa hilo kati ya Novemba 17, 2013 na Mei 2, 2019 wakiwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Kakula, ambaye alisaidiana na Batilda Mushi, alidai mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Augustina Mmbando kuwa katika kipindi hicho, MC Pilipili na Clement walichapisha maudhui kwa kutumia televisheni ya mtandaoni  (online TV) inayojulikana kwa jina Mc Pilipili, bila kuwa na kibali cha TCRA.Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka lao, walikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo wakili wa utetezi Jebrah Kambole aliwaombea dhamana washitakiwa hao.

MC Pilipili na Clemence wameachiwa huru kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata na barua ambayo imepitishwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa, anakotokea mdhamini huyo.Kesi imeahirishwa hadi Mei 7, 2019.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post