MBUNGE HAONGA AACHIWA KWA DHAMANA


Mbunge wa Mbozi mkoani Songwe, Pascal Haonga ambaye alikamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo ameachiwa kwa dhamana.

Wakili wa mbunge huyo, Gaston Gatubindi amesema kuwa Haonga ameachiwa kwa dhamana na anatakiwa kuripoti kwa mpelelezi wa Mkoa wa Dodoma siku ya Alhamisi.


Amesema kabla ya kupewa dhamana polisi walikwenda nyumbani kwa mbunge huyo kufanya upekuzi kwa mujibu wa taratibu.

Aidha baada ya kupewa dhamana, Haonga alikwenda moja kwa moja bungeni kuendelea na kikao cha bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto..


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527