MTIBWA SUGAR WAIPA KICHAPO YANGA...MATUMAINI YA UBINGWA YAZIDI KUFIFIA

Matumaini ya ubingwa yamezidi kufifia Yanga SC baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar mchana wa leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kiboko ya Yanga SC leo alikuwa ni chipukizi Riphat Msuya aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 52 akitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Na kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 32 na kupandsa hadi nafasi ya nne kutoka ya tano, ikiiteremsha Lipuli FC ya Iringa.

Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 74 baada ya kucheza mechi 32, lakini baada ya kufungwa mechi ya nne leo inazidi kupoteza matumaini ya ubingwa.

Inafuatiwa na Azam FC yenye pointi 66 baada ya kushuka uwanjani mara 31 na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 60 kufuatia ushindi wa leo katika mechi ya 23 tu.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Issa Kajia, Ally Makarani, Salum Kihimbwa, Jaffar Kibaya, Riphat Msuya na Haroun Chanongo.

Yanga SC; Klaus Kindoki, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Papy Kabamba Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Thabani Kamusoko, Heritier Makambo, Erick Msagati na Raphael Daudi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527