Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Freddie Manento akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, ukanda wa AfrikaMashariki na Kati(nchi 11), Mchungaji Emanuel Pelote akizungumza na Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wakinunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Bi. Jusline Gilbert mkazi wa Bariadi akaingalia baadhi ya bidhaa za Wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa Chama hicho Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkubwa wa hicho unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
Na Stella Kalinga, Simiyu
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento, Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.
Manento amesema ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu.
“Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mkutano wetu wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya kujenga hosteli katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam wetu wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili ya huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento
Pamoja na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento amesema ATAPE imewekeza katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa, mikorosho, miti ya maparachichi ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari 10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji mwingine.
Amesema hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039 imewekezwa katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika eneo la mkutano
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema Mkutano wa ATAPE umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia kipato na kupata ujuzi mpya kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa kwenye mkutano huo.
“ Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali nimepata pesa, nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya Simiyu, hivyo ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea matukio kama haya ili tupate pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza mjasiriamali kutoka Bariadi.
Nao wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa Simiyu wametoa wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kujifunza na kujionea kazi mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata ujuzi na maarifa mapya ya kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua bidhaa mbalimbali.
“ Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika viwanja hivi waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za jumla na rejareja, laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje waone maana ujasiriamali unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali Esther Jichogo kutoka Jijini Dar es salaam.
Wanachama zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa 20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli mbiu “KUSONGA MBELE NA MUNGU” ambao utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe 16/04/2019 hadi 21/04/2019.