MZEE WA UPAKO 'ETI NINI? NIMEKUFA? NITABAKI KUWA JUU,NITABAKI KILELENI! | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 10, 2019

MZEE WA UPAKO 'ETI NINI? NIMEKUFA? NITABAKI KUWA JUU,NITABAKI KILELENI!

  Malunde       Wednesday, April 10, 2019
Mchungaji wa kanisa la Maombezi la GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’

Kupitia video fupi iliyosambaa mtandaoni, Mchungaji wa kanisa la Maombezi la GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’, amejibu taarifa za kuzushiwa kifo, na kusema kuwa yeye hajafa.

Akionekana mzima wa mwenye afya Mzee wa Upako alisema haya;

“Eti nini!?, nimekufa!?. Mimi sijafa, wala siumwi hata mafua, niko mzima, watu wangu wote muwe na amani, eti nini!!? nimekufaa!!. Nitabaki kuwa juu, nitabaki kileleni.”

Mchungaji Lusekelo alimalizia taarifa hiyo huku akipiga kionjo cha Piere Mzee wa Liquid, huku akifurahi. 

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Mchungaji huyo hali yake ni mbaya kiafya, huku zingine zikisema kuwa amefariki dunia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post