Makubwa Haya! MWANAMKE AKUTWA NA NYUKI WANNE WAKIISHI NDANI YA JICHO LAKE

Mwanamke mmoja nchini Taiwan amekutwa na nyuki wanne wa sukari waliokuwa wakiishi ndani ya jicho lake , kikiwa ni kisa cha kwanza katika kisiwa hicho.


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 , aliyejulikana kama bi He, alikuwa aking'oa mizizi wakati nyuki hao walipoingia katika macho yake.

Daktari Hong Chi Ting wa chuo kikuu cha hospitali ya Fooyin aliambia BBC kwamba alishangazwa wakati alipowatoa wadudu hao kwenye macho.

Bi He ametolewa hospitalini na anatarajiwa kupona kabisa. Nyuki wanaofuata jasho huvutiwa na jasho na mara nyIngine huwarukia watu ili kunywa jashoi

Pia hunywa machozi ili kujipatia protini kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha kansas kuhusu wadudu.
'Wote walikuwa hai'

Bi He alikuwa akipalilia makaburi ya watu wa jamii yake wakati nyuki hao waliporuka na kuingia katika jicho lake la kushoto.

Wakati upepo ulipompiga usoni mwake alidhani kwamba ni uchafu uliokuwa umeingia , aliambia maripota.

Alikuwa akitembelea kaburi hilo kuadhimisha sherehe ya ufagiaji wa kaburi la Qing Ming ambayo huadhimishwa kwa kufagia makaburi ya watu unaowaependa.

Lakini saa chache baadaye macho yake yalikuwa yamefura yakiwa na uchungu mwingi, swala lililomshinikiza kwenda hospitalini ili kupata matibabu kusini mwa Taiwan.

''Hakuweza kufunga jicho lake kabisa'' .

''Niliatazama kwa kutumia darubini na kuona kitu cheusi kilichofanana na mguu wa mdudu'', Daktari Hong ambaye ni profesa aliyesomea magonjwa ya macho katika hospitali hiyo aliambia BBC.

''Niliushika mguu huo na polepole nikamtoa nyuki mmoja , na baadye nikamuona mwengine , na mwengine na mwqengine. Wote walikuwa wazima''.

Picha za nyuki hao zilionyeshwa katika runinga ya Taiwan.

Dkt. Hong aliongezea kuwa nyuki hao huenda walipeperushwa ndani ya jicho lake na upepo uliochanganyika na vumbi na kusalia ndani ya jicho la mwanamke huyo.

Nyuki hawa huwa hawashambulii binadaamu lakini wanapenda kunywa jasho, hivyobasi ndio wakapewa jina hilo, aliongezea.

Dkt Hong aliongezea kwamba bi He alikuwa na bahati kwamba hakufuta macho yake wakati nyuki hao walipoingia ndani.

''Alikuwa akivaliia miwani inayoshikana na macho hivyobasi kuweza kuharibu miwani hiyo. Iwapo angejaribu kujikuna jicho angewafanya wadudu hao kutoa sumu , pengine angekuwa kipofu''.

Nyuki hao bado ni wazima kwa sasa Dkt huyo anasema na watafanyiwa utafiti . Hii ni mara ya kwanza nchini Taiwan kitendo kama hicho kufanyika.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post