Wednesday, April 3, 2019

SPIKA NDUGAI AANIKA MADENI YA MBUNGE GODBLESS LEMA.....AMTIMUA MBUNGE WA CHADEMA

  Malunde       Wednesday, April 3, 2019
Spika Job Ndugai ameagiza Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), afike mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge leo saa 8:00 mchana kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharau na kulidhalilisha Bunge.


Spika amesema kuwa Bunge analoliongoza si dhaifu na yeyote atayeingia kwenye 18 zao anaalikwa kwenye mchezo huo.

Aidha, amesema huwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini ana msongo wa mawazo kwani tangu aingie Bungeni, amekopa Tsh. Milioni 644.“Yapo mambo ambayo hawasemi wacha tuseme kidogo amekopa Sh 644 milioni…Sasa hivi ameshalipa lipa zimefika Sh 419 milioni huu ni msongo wa mawazo ndio maana anafika mahali anajilipua tu na kadhalika,”amesema.

Katika hatua nyingine amemfukuza ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko(CHADEMA) baada ya kupiga kelele kumpinga kiongozi huyo kutaja deni la Lema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post