SERIKALI YAIKATALIA KENYA KUJENGA MABWAWA YA UZALISHAJI UMEME KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, April 29, 2019

SERIKALI YAIKATALIA KENYA KUJENGA MABWAWA YA UZALISHAJI UMEME KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

  Malunde       Monday, April 29, 2019

Serikali imeikatalia Kenya kujenga mabwawa ya uzalishaji umeme katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hayo yamesemwa leo Aprili 29, Bungeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Molel (CCM), ambaye alitaka kujua Tanzania inachukua hatua gani kuhusu suala hilo.

Katika swali lake Amina amesema kuna taarifa kwamba nchi ya Kenya inatarajia kutekeleza mpango wa kujenga mabwawa makubwa kwa ajili ya uzalishaji umeme ambao unatishia ustawi wa uwepo wa hifadhi ya Serengeti.

Akitoa majibu ya swali hilo Kanyasu amesema uchunguzi ulibaini utekelezaji wa miradi hiyo ungesababisha athari kubwa kwa ikolojia ya hifadhi hiyo na utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Kenya kuhalalisha miradi hiyo hazikuwa sahihi.

Aidha Kanyasu amesema miongoni mwa athari hizo ni pamoja na kuhatarisha ustawi na maisha ya viumbe hai kutokana na ukosefu wa maji katika Mto Mara wakati wa Kiangazi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post