RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA MAPARACHICHI

Rais Magufuli amezindua kiwanda cha Maparachichi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambapo amewaahidi wawekezaji wa Kiwanda hicho kurejesha VAT zinazodaiwa na wawekezaji baada ya  zoezi la uhakiki kukamilika.

Amesema, Serikali ilizuia kurejesha fedha hizo kutokana na wawekezaji wengi waliwasilisha madeni hewa na hivyo kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Aidha Rais Magufuli amemuomba mwekezaji huyo kuwafikiria wakulima kuhusu suala la nyongeza ya bei ya zao lao pamoja na mshahara kwa wafanyakazi. 

==>>Msikilize hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post