RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Dkt. Oscar Albano Mbyuzi.

Kufuatia uamuzi huo, Rais Magufuli amemteua Jimson Peter Mhagama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa ni kuwa uteuzi wa Mhagama unaanza leo tarehe 09 Aprili, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post