NYOKA WAVAMIA OFISI YA RAIS WA LIBERIA GEORGE WEAH

Nyoka wamepatikana katika ofisi ya rais wa Liberia George Weah , hatua iliomshinikiza kutoroka katika afisi yake na kufanya kazi katika afisi ya kibinafsi.

Tatibu wa masuala ya habari Smith Toby aliambia BBC kwamba siku ya Jumatano nyoka wawili weusi walipatikana katika jumba la ofisi ya wizara ya masuala ya kigeni .

Wafanyakazi wote wametakiwa kutoingia katika ofisi hiyo.

''Ni kuhakikisha kuwa wadudu wote wanaotambaa na kutembea wanaangamizwa katika jumba hilo'', alisema bwana Toby.

''Wizara ya maswala ya kigeni ndio ilio na ofisi ya rais, hivyobasi ikalazimika kuandika barua ikiwasihi wafanyikazi kusalia nyumbani huku wakiendelea kuweka dawa hiyo'', alisema.

Kanda ya video iliochapishwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la African News ilionyesha wafanyikazi wakijaribu kushambulia nyoka wakati walipoonekana katika eneo la kukaribisha wageni la jengo hilo.

''Nyoka hao hawakuuliwa'' , bwana Toby alisema. ''Kulikuwa na shimo mahali fulani ambalo walitumia kurudi''.

Maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa rais walionekana wakiyalinda makao ya bwana Weah katika mji mkuu wa Monrovia .

Msafara wa magari wa rais huyo ulionekana umeegeshwa nje ya jumba hilo.

Bwana Toby alisema kuwa wizara ya maswala ya kigeni ilianza kunyunyiza dawa hiyo siku ya Ijumaa.

''Jumba hilo limekuwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa sasa kwasababu yamfumo wa maji taka , hivyobasi kuna uwezekano wa nyoka kuingia katika jumba hilo'', alisema.

''Rais anarudi katika ifisi yake rasmi siku ya Jumatatu baada ya dawa hiyo kunyunyizwa iwapo nyoka hao watapatikana na kuuawa au la'', alisema bwana Toby.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527