JAMAA ALIYEKOSEA WAKATI WA KUPIGA KURA AJIKATA KIDOLE..AJUTA KUCHANGANYA NEMBO YA VYAMA

Jamaa mmoja aitwaye Yogesh Kumar Singh nchini India amekikata kidole chake cha shahada baada ya kugundua alipigia chama kisichofaa kura kwenye Uchaguzi Mkuu unaoendelea nchini humo. 

 Jamaa huyo alitaka kumpigia kura mtu aliyesimama kwa chama chenye nembo ya ndovu lakini aliishia kumpigia wa chama chenye nembo ya yungiyungi 

Yogesh Kumar Singh alisema alinuia kukipigia kura chama anachofahamu sera zake lakini nembo zilimchanganya na badala yake akakipigia chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP). 

Yogesh Kumar Singh alisema alikasirika baada ya kupigia chama kisichofaa kura na hatimaye akaamua kujikata kidole cha shahada. 

Katika ripoti ya BBC, Kumar alipiga kura yake Alhamisi, Aprili 18, katika jimbo la Bulandshahr, Kaskazini mwa Uttar Pradesh. Hii ilikuwa ni katika awamu ya pili ya kura hiyo kwenye uchaguzi mkuu huo.

 "Nilitaka kupigia ndovu lakini nikapigia ua kimakosa," Kumar alisema katika video ambayo imesambaa mno mtandaoni. 

Alikuwa akitaja nembo za vyama zilizowekwa kwenye mashine za kupigia kura karibu na jina na mwaniaji. 

Nembo ya BJP ni yungiyungi, ndovu ni nembo ya chama cha Bahujan Samaj (BSP), chama kikubwa kinachoshirikiana na vyama vingine viwili vya majimbo dhidi ya BJP. 

Nembo kwenye uchaguzi huo ni muhimu sana hasa ikizingatiwa idadi ya watu katika maeneo mbalimbali nchini India wasiojua kusoma na kuandika, wawaniaji wengi na vyama vya vingi vya majimbo na miungano huwachanganya sana wapiga kura.

Baada ya kupiga kura, kila kidole cha shahada hutiwa wino ili kuzuia uwezekano wa watu kupiga kura mara zaidi ya moja. 

Uchaguzi huo unafanywa katika awamu zaidi ya saba, huku kura zikitarajiwa kuanza kuhesabiwa Mei 23,2019.

 Kuna wapiga kura halali 900 milioni wanaoshiriki na idadi hiyo inafanya kura hiyo kuwa kubwa zaidi duniani. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post