MAITI YA BINTI YAFUKULIWA KABURINI KISHA KUBAKWA DAR | MALUNDE 1 BLOG

Friday, April 12, 2019

MAITI YA BINTI YAFUKULIWA KABURINI KISHA KUBAKWA DAR

  Malunde       Friday, April 12, 2019
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa aliyekuwa Ofisa wa Wizara ya Madini, Mery Mkwaya Maramo (35) aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii na kuzikwa jana katika makaburi ya Pugu-Mwakanga jijini Dar es Salaam, umefukuliwa na kutolewa nje ya jeneza kisha kuvuliwa nguo usiku wa kuamkia leo, Ijumaa, Aprili 12, 2019 na watu wasiojulikana.

Kaka wa marehemu Mary aitwaye Deogratius Maramo, amedai mwili wa marehemu uliingiliwa kimwili baada ya kutolewa nje na umekutwa umechanuliwa miguu, lakini bado wanasubiri ripoti ya polisi ili kujua kilichotokea kwani hakuna kitu chochote kilichoibiwa katika kaburi hilo.

Mramo anasema kuwa baada ya kufika makaburini hapo walifika kwa mwenyekiti wa mtaa ule ili kutoa taarifa ambapo hata wenyeji wa eneo hilo walishangazwa na kitendo hicho na kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Kwa upande wake mwangalizi wa sehemu ya makaburi hayo ambayo yanamilikiwa na Kanisa Katholiki, Mzee Hela Mwenzigeje amesema kuwa kitendo hicho ni mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo na kimewatia doa.

Aidha wakazi wa eneo hilo wameomba watu wa Kanisa waweke uzio katika eneo hilo ili kuondoa wasiwasi uliotanda miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post