PAPA AWABUSU MIGUU RAIS KIIR, MACHAR KUHAMASISHA AMANI

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini.

Amechukua hatua hiyo jana Alhamisi Aprili 11,2019 kama ishara ya kuwahamasisha viongozi hao kuuendeleza mchakato wa amani ili taifa hilo lirejee katika utulivu.

Papa Francis alimuomba Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir pamoja na hasimu wake, Rieck Machar kuendeleza mazungumzo ya amani, licha ya kuongezeka kwa ugumu na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya makamu wa Rais Rebecca Nyendeng Garang.

Mara kwa mara Papa Fransis amekuwa akifanya tendo la kiutamaduni linaloendana na imani la kuwaosha wafungwa miguu kila inapofika Alhamisi Kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa.

Akizungumza na viongozi hao walikuwa na ziara ya siku mbili ya kiroho Vatican, Papa Francis alisema anatarajia kusitishwa kwa uadui, mapigano na mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post