KIM JONG UN AKUBALI KUKUTANA TENA NA TRUMP, LAKINI KWA MASHARTI

Rais wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un amesema yuko tayari kwa ajili ya mkutano wa tatu na Rais wa Marekani, Donald Trump, lakini kwa masharti yakuridhisha pande zote mbili na kutatua mgogoro wa kidiplomasia wa silaha za nyuklia.


Rais Kim aliyasema hayo katika hotuba yake kwa  Bunge la hapa  juzi  saa kadhaa baada ya Rais  Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae-in mjini Washington Marekani na kujadili umuhimu wa mazungumzo na Korea Kaskazini, kuhusu silaha za nyuklia.

Katika mkutano wao huo wa mwishoni mwa wiki mjini Washington, Rais Trump alimwambia Moon kwamba yuko tayari kwa ajili ya  mkutano wa kilele wa tatu na Rais Kim, lakini Marekani itaendelea kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya kiuchumi.

Kim alirejea tena matamshi yake ya awali kwamba katika hotuba yake bungeni na kusema uchumi ulioporomoka wa nchi hii  utaendelea kujikongoja licha ya vikwazo vikali vya kimataifa ilivyowekewa kutokana na mpango wake wa silaha za kinyuklia na kwamba hatoshikilia kufanya mikutano na Marekani kwa lengo la kutaka kuondolewa vikwazo.

Rais Kim aliwahimiza Wakorea kujijengea uwezo wa kujitegemea ili waweze kupambana na kile alichokieleza kuwa nguvu ya maadui  wanaoamini nchi hii  inaweza kusambaratishwa kwa kutumia vikwazo.

“Sisi hakika tunaunga mkono suala la kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo na majadiliano. Lakini mtindo wa Marekani wa mazungumzo wa kulazimisha kwa masharti hautufai sisi, wala hatuna haja nao,” alisema  Rais Kim wakati wa hutuba yake hiyo.

 Kwa mujibu wa  Shirika Kuu la Habari la hapa, KCNA, Kim alisema kusambaratika kwa mkutano wa kilele uliotakiwa kufanyika Februari mwaka  huu  kulitokana na kile alichokieleza kama masharti ya Marekani ya upande mmoja, ambayo alisema yalimpa wasiwasi iwapo nchi hiyo  ina nia ya kweli ya kuimarisha uhusiano kati yao.

Hata hivyo Rais  Kim aliongeza kwamba uhusiano wake binafsi na Rais Trump ni mzuri na wanaweza kutumiana barua wakati wowote.

Trump na Kim walikutana mara mbili ambapo mara ya kwanza ilikuwa Hanoi mji mkuu wa Vietnam mnamo mwezi Febuari na mara ya pili ilikuwa Singapore mwezi Juni mwaka jana.

Mara zote mbili walishindwa kufikia makubaliano ya mkataba wa Marekani kuondolea vikwazo vya kiuchumi Korea Kaskazini ili nchi hiyo nayo kwa upande wake iachane na mpango wake wa kutengeneza silaha za kinyuklia pamoja na makombora.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527