JANGILI AKANYAGWA NA TEMBO KISHA KULIWA NA SIMBA AKIWINDA FARU


Mtu mmoja aliyesadikiwa kuwa ni jangili wa wanyama aina ya faru ameuawa na Tembo kisha kuliwa na Simba katika hifadhi ya taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mamlaka ya utafiti nchini humo, baada ya uchunguzi imeweza kugundua fuvu pamoja na masalia ya nguo ya mtu huyo.

Pia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini ilisema Ijumaa kuwa jangili huyo pamoja na washirika wenzake wanne walikuwa wakijaribu kuwinda wanyama aina ya faru, jioni ya Jumanne, ambapo washirika hao waliiambia familia ya marehemu kuwa mwenzao ameuawa na Tembo.

Mkurugenzi wa hiadhi hiyo ametoa salamu za rambirambi kwa familia huku akitoa angalizo kuwa, ''kuingia kwenye mbuga ya Kruger kinyume cha sheria na kwa miguu si jambo jema,'' alisema Murugenzi huyo. ''ni mbuga yenye hatari nyingi na tukio hili linadhihirisha hayo''.

Hifadhi ya Kruger imekua ikikabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe za faru kwenye nchi za bara la Asia. 

Nchi ya Afrika Kusini ina takribani faru 20,000, ambayo ni asilimia 80 ya faru wote wanaopatikana dunia nzima. Tangu mwaka 2008, jumla ya faru 7,000 wamewindwa kinyume na utaratibu nchini humo, ambapo 1028 kati yao wakiuawa katika mwaka 2017 pekee.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post