BABA MZAZI MATATANI KWA KUBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA MINNE

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mkazi wa Kata ya Nyankumbu, Selemani Mathias (35), kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka minne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema mtuhumiwa huyo yuko rumande akisubiri uchunguzi tuhuma dhidi yake ukamilike ili aweze kufikishwa mahakamani.

Alisema mtoto huyo alikuwa akiishi na baba yake baada ya mama yake kutengana na baba yake na kumwacha mtoto huyo na mdogo wake wa miaka miwili.

“Siku ambayo unyama huo ulipofanyika mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wa jirani na baada ya kucheza walikwenda nyumbani kwa hao majirani na ndipo mtoto wa mama wa jirani huyo alipomwambia mama yake kuwa rafiki yake alikuwa anajikuna kila wakati sehemu za siri,” alisema Kamanda Mponjoli.

Alisema baada ya mama huyo wa jirani kusikia hivyo alimwita mtoto huyo na kuanza kumuhoji kwa nini anajikuna na ndipo mtoto huyo alipoeleza jinsi baba yake alivyomuingilia.

“Hatutapenda kumtaja jina huyu mama jirani kwa kuwa anatusaidia upelelezi na alifafanua kuwa mtoto huyo alisema mara baada ya kumbaka baba huyo alimtishia kumuua iwapo atatoa siri hiyo kwa watu,”alisema.

Ilidaiwa kuwa kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya wazazi hao, mama wa watoto hao aliamua kuhama nyumbani hapo na kuwaacha watoto wakilelewa na baba yao pekee hali ambayo ilionekana kuchangia kutendeka kwa unyama huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527