Sunday, March 31, 2019

RAIS MAGUFULI AMPA KAZI NDUNGURU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

  Malunde       Sunday, March 31, 2019

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia sera.

Taarifa  iliyotolewa leo Jumapili Machi 31, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Ndunguru ameteuliwa kushika nafasi hiyo kujaza nafasi iliyokuwa wazi.

Imesema kabla ya uteuzi huo, Ndunguru alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kufuatia Uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Kabla ya uteuzi huo, Mbibo alikuwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Jumapili Machi 31, 2019.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post