REDEOA YATOA TUZO KWA HALMASHAURI,MANISPAA NA MAJIJI YALIYOFANYA VIZURI MTIHANI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Umoja wa Maafisa Elimu wilaya na mikoa Tanzania Bara [REDEOA]umetoa tuzo kwa halmashauri na majiji mbalimbali yaliyofanya vizuri  2018  katika upimaji wa mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia  shule za msingi na   sekondari.

Akitangaza tuzo hizo jijini  Dodoma Machi 27  zilizotolewa na  mkurugenzi wa REDEOA  Benjamin  Oganga,Katibu mkuu wa REDEOA  Bw. Efraim Majinge ,amezitaja halmashauri  10 zilizofanya vizuri matokeo ya Darasa la nne 2018 , ya kwanza ni Arusha Manispaa,ya pili ni Muleba Kagera,Ya tatu ni  Moshi Manispaa,ya nne ni Ilala ,Halmashauri ya tano ni Ulanga,ya sita ni Makambako ya saba ni Korogwe ,ya nane ni Misenyi Kagera ,tisa ni Ilala jiji na nafasi ya kumi ni manispaa ya Bukoba.

Kwa Darasa la saba 2018 ya kwanza ni Arusha,ya Pili ni Moshi Mkoani Kilimanjaro,nafasi ya tatu ni Kinondoni Dar  es  Salaam, ya nne ni Ilala Dar es Salaam, ya Tano ni Chato Geita,ya sita ni Ilemela Manispaa ,ya  saba ni Mafinga Iringa, nafasi ya nane ni Hai Kilimanjaro ,nafasi ya tisa ni Jiji la Mwanza nafasi ya kumi ni Kigamboni Dar es Salaam.

Katika kidato cha pili,halmashauri kumi zilizofanya vizuri 2018 ,ya kwanza ni Bagamoyo,nafasi ya pili Bukoba mji Kagera,ya tatu njombe mji,ya nne Meru Arusha,nafasi ya tano Longido Arusha,nafasi ya sita Biharamulo Kagera,ya Saba ni Kasulu mji,Kigoma,ya nane ni Morogoro Manispaa ,ya tisa ni Monduli Arusha na nafasi ya Kumi Kibaha Mji Pwani.

Halmashauri  kumi zilizopata tuzo kwa  matokeo Mazuri ya Kidato cha nne 2018 ,ya kwanza ni Bagamoyo  Pwani,ya pili Bukoba mji Kagera,  ya tatu ni Kahama mji Shinyanga,ya nne Kibondo Kigoma ,ya tano ni Babati Mji Manyara,ya sita ni Meru Arusha,ya Saba ni Kibaha Pwani ,nafasi ya nane ni Njombe mji,ya tisa ni Bariadi Simiyu na nafasi ya kumi ni Igunga Tabora.

Na katika upimaji  Darasa la nne mikoa yote 26   Tanzania Bara wana umoja wa REDEOA zilivuka Malengo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527