MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA AKUTWA AMEUAWA SHAMBANI


Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjori Mwabulambo

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Yungwe wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuawa kwenye eneo la kichaka huku sababu za kifo hicho zikiwa bado hazijajulikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masono aliomba ruhusa ya kwenda nyumbani kwao Ukerewe kwa ajili ya matibabu kutokana na hali ya afya yake kutokuwa nzuri.

Amesema,marehemu alipewa ruhusa na kuondoka kwenda nyumbani na alivyomaliza matibabu February 28 mwaka huu alirejea shuleni na kuendelea na masomo yake.

Aidha,Kamanda Mponjoli amesema tangu Machi Mosi mwezi huu mwanafunzi huyo alitoweka shuleni pia hakuonekana katika maeneo ya nyumbani ambapo alikuwa amepanga.

Sanjari na hayo, Kamanda amesema ilipofika tarehe 8 mwezi huu mama mmoja ambaye jina lake halikujulikana, wakati akiwa shambani analima aliona fuvu la binadamu kwenye eneo la shamba lake hali iliyomshtua na kupelekea kuwaita wananchi na walipofika na kuchunguza walibaini kuwa ni mabaki ya nguo za shule kuwepo kwenye eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527