MHUBIRI ATAKA WANAUME WAWALIPE MISHAHARA WAKE ZAO KWA KAZI WANAZOFANYA NYUMBANI


Mhubiri mmoja kutoka Ghana Ekow Badu Wood amewataka wanaume wote ulimwenguni mzima kuwalipa mshahara wanawake wao kwa ajili ya kazi wanazozifanya nyumbani.

Kwa mujibu wa mhubiri huyo wanawake hutekeleza majukumu mengi nyumbani na kuhakikisha wanadumisha amani katika jamii hivyo ni vyema kuwalipa mshahara kila mwezi ili kuwapa motisha ya kuboresha nyumba zao zaidi 

" Njia moja ya kutoa shukrani kwa wanawake ni kuwalipa mshahara kila mwezi, hii ni kwa ajili ya kazi ambazo hufanya ili kuboresha ndoa zao, malipo hayo yatawafanya wawe na motisha zaidi," Mhubiri huyo alisema.

 Mhubiri huyo alisisitiza kuwa kila familia hunawiri panapo mwanamke na hivyo wanapaswa kutambulika na kutuzwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527