KUTANA NA HOTELI YA KWANZA ILIYOPO ANGA ZA JUU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 9, 2019

KUTANA NA HOTELI YA KWANZA ILIYOPO ANGA ZA JUU

  Malunde       Saturday, March 9, 2019
Ilinuiwa kusisimua safari za duniani: Kituo cha Aurora hoteli ya kwanza duniani - kwenye mzunguko wa obiti katika anga za juu.

Tangazo rasmi kuhusu mpango huo lilitolewa Aprili mwaka jana huko San Jose, California Marekani.

Imejengwa kwa ukubwa wa ndege kubwa ya kibinafsi, itakayoruhusu watalii kupaa maili 200 juu ya ardhi ya dunia, na kupata fursa ya kutupia jicho mandhari ya sayari na muanga wa kaskazini na kusini.

Gharama sio nyepesi: safari hiyo ya siku 12 kwenye kituo cha Aurora inayotarajiwa kufanya ziara ya kwanza yakitalii mwaka 2022, ni ya thamani ya $9.5m kwa mtu mmoja.

Hatahivyo, kampuni hiyo inasema orodha ya watu wanaosubiri safari hiyo ya kitalii inakusanywa miezi 7 kabla ya safari yenyewe.

"Sehemu ya hisia tunayotaka kuwapatia watu ni kujua maisha halisi ya mwana anga za juu yalivyo," amesema Frank Bunger, muasisi na mkurugenzi mtendaji wa Orion Span, kampuni inayosimamia uidhinishaji wa hoteli hiyo ya Aurora.

"Lakini tunatarajia wageni wengi watakuwa wakichungulia nje ya madirisha , na kuwaita kila wanaowajua, na iwapo watachoka, tuna tunachokita 'holodeck,' mfumo wa uhaisia unaoonyesha hali ilivyo, na unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya mfano kuelea katika anga za juu, kutembea kwenye mwezi na hata kucheza gofu."
Kando na kuweza kuchungulia nyota na sayari ya duni kutoka dirishani. inatarajiwa wageni katika Aurora watajaribu kufanya mambo tofuati katika muda watakaokuwa wakiishi katika hoteli hiyo, kama kujaribu kupanda chakula kama inavyofanywa sasa na maafisa katika ISS.

Wengi katika taaluma ya sayansi wanaona kama hatua isiyoepukika katika maisha ya mwanadamu. Lakini kuna na msemo wa kale, kwamba jihadhari kabla ya hatari; kusema kwamba safari ya raia kwenda katika anga za juu ni kitu kilicho katika kiwango cha msingi, bado haielezi hatua imepigwa kiasi gani.
Kila mmoja anakubali kwamba utalii katika anga za juu ni jambo kubwa: ulianza mnamo 2001 wakati raia wa Marekani Dennis Tito alipolilipa shirika la anga za juu Urusi $20m ili kuzuru kituo cha ISS kilichopo huko. baadhi ya mataifa tayari yameidhinisha msingi katika sekta hiyo katika siku zijazo.

Lakini wataalamu wanasubiri kuona iwapo utalii wa raia katika anga za juu unaweza kutekelezwa na kwa namna gani.

Kilichosalia kubainishwa ni usalama, na viwango vya uhandisi kwa mfumo wa usafiri wa raia katika anga za juu.

Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post