MADIWANI WA MAGU WAMWIMBUKIA LOWASSA


Lowassa akiwa na baadhi ya madiwani Halmashauri ya Magu

Siku chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kutangaza kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukaa ndani ya upinzani kwa takribani siku 1312 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiongozi huyo ameanza kupewa fursa.

Fursa ambayo kiongozi huyo ameipata ni kutembelewa na madiwani kutoka Halmashauri ya Magu mkoani Mwanza ambao walifika ofisini kwake Mikocheni Dar es salaam kwa ajili ya kumuomba kutembelea halmashauri hiyo.

Wakizungumza mbele ya kiongozi huyo, Madiwani walimuomba Lowassa kutembelea Jiji la Mwanza baada ya uamuzi wake wa kurejea chama tawala ikiwa pamoja na kuhamasisha hali ya ukusanyaji wa mapato kwenye jiji hilo.

Wakati akipokelewa na uongozi mkuu wa CCM, Marchi 1, 2019 Lowassa mwenyewe hakubainisha nini sababu ya kurejea CCM, bali aliishia kusema kuwa amerudi nyumbani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527