Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza na wananchi waliofika kwa ajili ya kuwasilisha kero juu ya Ardhi katika ukumbi wa mikutano wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Hai mjini.



Baadhi ya wananchi waliofika kuwasiliha kero zao.







Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini.
Serikali katika wilaya ya Hai imetangaza kubatilisha umiliki wa viwanja 34 kati 52 vilivyopo kwenye eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kutokana na madai mbalimbali ikiwemo kutoyaendeza.
Madai mengine ya kuandikwa kwa ilani hiyo kwa Waziri wa Ardhi, , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetajwa kuwa ni wamiliki wa maeneo hayo ni deni la fedha za Pango la Ardhi kwa zaidi ya miaka 20.
Wanaotajwa kumiliki maeneo hayo wamo pia viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa serikali wastaafu,wafanyabiashara ,kampuni zinazo miliki mashamba makubwa pamoja na taasisi zisizo za kiserikali.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa kushughulikia kero zinazohusu masuala ya Ardhi ,Mkuu wa wilaya ya Hai ,Lengai Ole Sabaya amesema tayari Halmashauri imewasilisha barua kwa Waziri wa Ardhi ili kumfikishia rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania kwa ajili ya utiaji saini.
Idadi hiyo ya watu 34, inafanya jumla ya kiasi cha fedha kinachodaiwa kutokana na pango la ardhi kufikia Sh. 1, 828, 166, 096.
Waliotajwa katika orodha ya wamiliki wa viwanja hivyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe ,Mkuu wa mkoa wa zamani wa Kilimanjaro, Cynthia Hilda Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichopo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa mji wa Moshi na wamiliki wa shule binafsi na makampuni ya utalii.
Sabaya alisema watu hao wamo katika orodha ndefu ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa na kwamba kwa mujibu wa orodha hiyo, Kiwanda cha Mashine Tools kina deni la Sh. milioni 315,720,720 ambalo inadaiwa kati ya mwaka 2010 hadi 2018.
“Huko nyuma watu walipewa viwanja mashine tools, viwanja 52 vikubwa wakaambiwa waendeleze kwa sababu ni eneo la viwanda, wana miaka mingapi? Afisa Ardhi yuko wapi, njoo, nini kimetokea pale.
“Sasa sikilizeni huo mziki, unapewa shamba (eneo la kiwanja) mwaka 1984, mmesikia? kabla mimi sijazaliwa, hajawahi kufanya lolote, akapewa na halmashauri ili waendeleze kujenga viwanda. Sasa Afisa Ardhi ameshaandika barua ya kubatilisha hivyo viwanja…Niwaambie hapa hapa wako watu mnaowaheshimu na hawalipi kodi na leo ntawataja humu.”
Katika mkutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya alipokea malalamiko 266 yanayohusu ardhi na kuahidi ndani ya siku mbili yatakuwa yamepata majibu.
Katika mkutano huo, Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Alphonce Lekule, aliwaeleza wananchi wa Hai kwamba kuwapo idadi kubwa ya malalamiko ni kwa ni changamoto kwa watendaji wa ardhi.
Social Plugin