DPP ADAI RUFANI YA MBOWE NA MATIKO HAINA MASHIKO......MAWAKILI WAO WAPANGUA HOJA, MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KESHO

Mawakili wa upande wa Freeman Mbowe na Ester Matiko, Peter Kibatala na Jeremia Mtobesya wameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwarejeshea washtakiwa hao dhamana yao na kwamba rufani yao ina mashiko ya kisheria.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Sam Rumanyika inasikiliza rufani ya walalamikaji Mwenyekiti Taifa wa Chadema,Freedman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko wakipinga Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana.

Kibatala amedai Mahakama ya Kisutu ilikosea kufuta dhamana ya walalamikaji na kwamba hakukua na hoja za msingi za kufanya hivyo.

Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ambaye ni mlalamikiwa katika rufani hiyo ameiomba mahakama Kuu kutupilia mbali rufani hiyo kwa sababu haina mashiko maana walalamikaji walikiuka masharti ya dhamana.

DPP amesema sababu za wadhamini na walalamikiwa kushindwa kueleweka na mahakama ya Kisutu ni sababu zilizosababisha kutenguliwa dhamana hiyo, hivyo uamuzi huo ulikuwa halali kwa kuwa kutokufika kwao mahakamani kumesababisha kesi kushindwa kuendelea kusikilizwa.

Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza hoja za rufani kwa pande zote mbili amesema atatoa uamuzi wake kesho saa 7:00 mchana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527