KAMPUNI YA HUDUMA ZA BIMA YA HOWDEN PURI YAZINDUA HUDUMA ZAKE TANZANIA


Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya huduma za Bima ya Howden (kulia) iliyopo chini ya Kampuni mama ya Hyperion Insurance Group , David Howden akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Howden Puri Insurance Brokers nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana,wengine pichani kutoka kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke,Afisa Mtendaji Mkuu wa Howden Puri nchini, Umesh Puri na Mwenyekiti wa Howden Kanda ya Afrika, Pravceen Vashista.
Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo wengine pichani ni Maofisa Waandamizi ya Howden Puri
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akihutubia wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya huduma za Bima ya Howden, David Howden akihutubia wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA , Adelaida Muganyizi (Kushoto) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Howden, , David Howden wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio na kubadilishana mawazo.

Kampuni ya kimataifa ya huduma za bima ya Howden, chini ya kampuni mama ya Hyperion Insurance Group imeingia katika ushirikiano wa kimkakati wa kukuza biashara na kampuni kongwe ya masuala ya bima nchini ya B.R. Puri & Company Limited, ambapo chini ya ushirikiano huo imeanzishwa kampuni itakayoendesha biashara zake nchini inayojulikana kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited.

Hafla ya uzinduzi wa kampuni hii mpya umefanyika katika ubalozi wa Uingereza nchini jijini Dar es Salaam.

David Howden, Afisa Mtendaji Mkuu wa Hyperion na Howden amesema “Hii ni hatua nzuri kwetu kwa kampuni ya Howden kuwa na mshirika wa kibiashara barani Africa na tunayo furaha kushirikiana kibiashara na kampuni ya B.R. Puri, ikiwa ni moja ya kampuni kubwa inayoongoza katika soko la Tanzania.

 Mikakati yake mikubwa ya kibiashara inaenda sambamba na mikakati ya Howden na tuna imani kwa kuunganisha mikakati yetu ya kibiashara kupitia kampuni mpya ya Howden Puri tutaweza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na jumuiya za kimataifa nchini Tanzania, Afrika Mashariki na zaidi ya hapo. Kupitia ushirikiano huu tunaona zipo fursa nyingi zinazotuwezesha kukua zaidi kibiashara”

Akiongelea ushirikiano huu wa kibiashara, Arun Puri, Mwenyekiti wa Howden Puri alisema “Kampuni ya BR Puri & Company, ilianzishwa na baba yangu kwenye miaka ya 1950, ikiwa ni moja ya kampuni ya kwanza nchini Tanzania kujishughulisha na biashara za uwakala wa bima.

 Naamini kwa kuunganisha ujuzi wetu na uzoefu mkubwa tulionao na utaalamu wa Howden wa kutoa huduma katika nchi nyingi duniani kutanufaisha wateja wetu tulio nao na watakaojiunga nasi.

Umesh Puri, Afisa Mtendaji Mkuu wa Howden Puri, aliongeza kusema “Tukiwa kampuni ya uwakala wa bima inayoangalia mbele hapa nchini Tanzania, lengo letu ni kubuni huduma mpya za bima zinazoendana na hali ya soko la Tanzania. 

Howden imechagua kushirikiana na kampuni ya Tanzania kibiashara ikiwa ni ya kwanza barani Afrika kutokana na jitihada nzuri zinazofanywa na wasimamiaji wa sekta ya bima kuiboresha zaidi sambamba na mazingira mazuri ya kufanyia biashara yaliyopo nchini kwa ujumla”.

Howden, kampuni ya uwakala wa huduma za bima iko chini ya kampuni mama ya Hyperion Insurance Group, na inatoa huduma za bima za aina mbalimbali kwa wateja kupitia mtandao wake sehemu mbalimbali duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post