CUF LIPUMBA WAMTEMA MAALIM SEIF...KATIBU MKUU SASA NI KHALIFA SULEIMAN | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 16, 2019

CUF LIPUMBA WAMTEMA MAALIM SEIF...KATIBU MKUU SASA NI KHALIFA SULEIMAN

  Malunde       Saturday, March 16, 2019

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtangaza Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Mbali na Khalifa, Profesa Lipumba pia amemtangaza mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya kuwa naibu katibu mkuu Bara na Fakhi Suleiman Khatibu kuwa naibu katibu mkuu Zanzibar.

Profesa Lipumba amemtangaza Khalifa ambaye ni mbunge wa zamani wa Gando kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad leo Jumamosi Machi 16, 2019 makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo mpya, amepatikana baada ya kuchaguliwa na Baraza Kuu la Uongozi lililokutana jana Ijumaa.

Hata hivyo, hatima ya viongozi hao wapya wa CUF akiwamo Profesa Lipumba aliyechaguliwa na mkutano mkuu Jumatano iliyopita Machi 14, 2019, itajulikana baada ya hukumu itakayotolewa Jumatatu ya Machi 18, 2019 na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ni ya kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachana wa chama hicho upande wa Maalim Seif wakipinga uhalali wa Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post