BALOZI WA ZAMBIA NCHINI KENYA AFARIKI DUNIA
Balozi wa Zambia nchini Kenya Brenda Muntemba-Sichilembe, amefariki dunia jijini Nairobi baada ya kupata ajali.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Macharia Kamau, amesema leo Jumatano Machi 20, 2019 kwamba balozi huyo alipoteza maisha baada ya kupata ajali ya gari barabara ya Machakos.

Amesema Mutemba (49), alipoteza maisha akipatiwa matibabu Hospitali ya Nairobi baada ya ajali iliyotokea wiki tatu zilizopita.

Kamau amesema balozi huyo alipata ajali Februari 26, 2019 eneo la Lukenya barabara ya Mombasa baada ya gari lake kugongana na gari kubwa la mizigo.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post