AS VITA WAICHAPA AL AHLY 1-0

Timu ya AS Vita imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Kundi D usiku wa leo Uwanja wa Martyrs de la Pentecote, zamani Kamanyola mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 19, Tuisila Kisinda dakika ya 84 akimalizia pasi ya Ducapel Moloko aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kazadi Kasengu.

Kwa ushindi huo, AS Vita inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tano ikirudi nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly yenye pointi saba pia za mechi tano, lakini inaongoza kundi kwa wastani wake mzuri wa mabao.

Simba SC ya Tanzania inaangukia nafasi ya tatu na pointi zake sita za mechi nne, kuelekea mchezo wa usiku huu mjini Bechar nchini Algeria dhidi ya wenyeji, JS Saoura wanaoshika mkia kwa pointi zao tano za mechi nne pia.

Kikosi cha AS Vita kilikuwa; Nelson Lukong, Yanick Bangala, Nelson Munganga, Makwekwe Kupa, Botuli Padou Bompunga, Glody Ngonda, Mukoko Tonombe, Fabrice Ngoma, Jean-Marc Makusu/ Jeremie Mumbere dk81, Kazadi Kasengu/Ducapel Moloko dk66 na Tuisila Kisinda/Michael Wango Ayitshela dk89.

Al Ahly; Mohamed El Shenawy/Aly Lotfy dk25, Ayman Ashraf, Saad Samir, Ali Maaloul, Mohamed Hany, Amr Al Sulaya, Ramadhan Sobhi/ Hussein El Shahat dk75, Karim Nedved, Nasser Maher, Marwan Mohsen/ Walid Azarou dk70 na Junior Ajayi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527