Picha : JESHI LA POLISI LAFUNGA MAFUNZO YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA SHINYANGA VIJIJINI



Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO) Emmanuel Palangyo amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa madereva wa vyombo vya moto 95 kutoka kata ya Puni, Tinde 33 ,Didia 59 na wanafunzi watatu.




Mafunzo hayo yamefungwa leo Machi 9,2019, zoezi lililofanyika kwenye shule ya Msingi Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) ambapo washiriki wa mafunzi hayo wamepewa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo ya udereva, yaliyotolewa ndani ya wiki moja na chuo cha udereva New Vision Vocational Traning Centre cha Jijini Dar es salam.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Palangyokwa niaba ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa madereva wa vyombo vya moto na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani.

“Naomba mafunzo haya ambayo mmeyapata yawe na tija katika kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani, kwa sababu mtakuwa mnazijua sheria na mzitii kwa vitendo pamoja na kuacha kutumia vilevi, na kuepuka kuendesha kwa mwendo kasi, vitu ambavyo vimekuwa vikichangia kwa asilimia kubwa kupata ajali" alisema Palangyo.

“Natoa tahadhari pia kwa madereva wazembe ambao wamekuwa wakivunja sheria za usalama barabarani, Jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria bila ya kuwa na huruma, ambapo natoa wito kwao nao wajiandikishe ili waje kupatiwa mafunzo haya ya kuzijua sheria za usalama barabarani ili tuendele kuwa salama,”aliongeza.

Naye mratibu wa mafunzo hayo ya udereva kutoka Chuo cha Udereva New Vision Vocational Traning Centre cha Jijini Dar es salam Deogratius Kidana, alisema wamekuwa wakitoa mafunzo hayo ya sheria za usalama barabarani mara kwa mara kwa madereva wa vyombo vya moto, wakiwemo na wale ambao wana leseni lakini hawakupitia mafunzo hayo.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokana na uzembe wa madereva kwa kutozijua sheria za usalama barabarani hasa waendesha bodaboda, ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na wengine kupata ulemavu.

Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo ya Sheria za usalama barabarani akiwemo Thabiti Matepet, walisema yatawasaidia kuwa makini barabarani hasa pale wanapokuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakijiendeshea tu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO) Emmanuel Palangyo akiwataka madereva ambao wamehitimu mafunzo ya sheria za usalama barabarani kuzitii sheria hizo kwa vitendo ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na wengine kuwapatia ulemavu.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mtaribu wa mafunzo ya Sheria za usalama barabarani Deogratius Kidana kutoka Chuo cha Udereva New Vision Vocational Traning Centre cha Jijini Dar es salam, akielezea lengo la mafunzo hayo ni kupunguza ajali za barabarani.
Wahitimu wa mafunzo ya sheria za usalama barabarani, wakisikiliza nasaha za mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga Emmanuel Palangyo, kuzitii sheria hizo na kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani.

Thabiti Matepet,ambaye ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo ya sheria za usalama barabarani akipongeza kutolewa kwa elimu hiyo ambayo itawasaidia kuepukana na ajali zisizo za lazima.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga Emmanuel Palangyo akigawa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo ya Sheria za usalama barabarani.

Mratibu wa mafunzo hayo ya sheria za usalama barabarani Deogratius Kidana, akipeana mikono ya pongezi na mhitimu wa mafunzo hayo Thabiti Matapet ambaye pia ni afisa tarafa wa Itwangi.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ya Sheria za usalama barabarani Wales Mhoka, akipeana mkono wa pongezi na muhitimu wa mafunzo hayo Richard Mwita.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga Emmanuel Palangyo akiendelea na zoezi la ugawaji wa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo ya Sheria za usalama barabarani.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ya sheria za usalama barabarani Wales Mhoka, akiendelea na zoezi la ugawaji vyeti kwa hitimu mara baada ya mgeni rasmi kuwapatia wale wahitimu ambao walipagwa kuwapatia vyeti hivyo huku na yeye akiendelea kwa wengine ambao walisalia kupewa vyeti hivyo.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527