ZANTEL YAANZISHA MPANGO WA WAFANYAKAZI WAKE KUSHIRIKI KUFANYA MAZOEZI YA KUJENGA AFYA ZAO

Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakishiriki kufanya mazoezi ya viungo chini ya mpango ulioanzishwa na kampuni ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kuongeza ufanisi kazini yaliyonduliwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel imeanzisha mpango, unaowawezesha wafanyakazi wake wote kushiriki kufanya mazoezi ya mwili baada ya saa za kazi kwa ajili ya kujenga afya zao.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Zantel Joan Makwaia Kazimoto amesema mazoezi hayo yanafanyika mara tatu kwa wiki baada ya saa za kazi, na wanafanya mazoezi ya viungo ya kucheza (Zumba), kutembea na aerobics.

“Zantel siku zote inawajali wafanyakazi wetu kama ambavyo inavyowajali wateja wake, ndio maana tumeanzisha mpango kama huu wa mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi wetu wote sambamba na kuleta tija na ufanisi, tunaamini wafanyakazi wenye afya bora wanatekeleza majukumu yao ya kazi ya kila siku vizuri”,alisema Joan.

Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel walipohojiwa waliuelezea mpango huo kuwa ni mzuri kwa afya zao pia unadhihirisha jinsi kampuni inavyowajali wafanyakazi wake kama ambayo imekuwa ikiwajali wateja wake.

Akiongea wakati wa mazoezi hayo, mmoja wa wafanyakazi wa Zantel, Gamdad Murad aliushukuru uongozi wa Zantel kwa kujali afya zao kwani ni muhimu zaidi hasa kazini na katika familia zao pia.

“Mazoezi haya yanatuhamasisha kubadilisha mfumo wetu wa maisha na pia kuanza kuwazoesha watoto wetu kufanya mazoezi katika umri mdogo ili kuepukana na magonjwa yanayoletwa na uzito kupita kiasi,” alisema Murad.
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakishiriki kufanya mazoezi ya viungo chini ya mpango ulioanzishwa na kampuni ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kuongeza ufanisi kazini yaliyonduliwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527