SHIRECU YAFANIKIWA KUWAHUDUMIA WAKULIMA WA PAMBA KWA MSIMU WA 2018/19

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Katika msimu wa pamba wa mwaka 2018/19 Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Region Co-Operative Union (1984) Ltd - SHIRECU) kimeweza kuwahudumia wakulima wa zao la pamba mkoa wa Shinyanga kupitia vyama vya msingi (AMCOS) kwa kuwapatia huduma zifuatazo: 

⇨Kufukiza dawa maghala ya vyama vya msingi (Fumigation): Hadi kufikia mwezi Mei 2018, jumla ya maghala 184 katika AMCOS 121 yalifukizwa dawa kwa ajili ya kuhifadhi pamba katika msimu wa 2018,katika halmashauri za Kishapu,Shinyanga manispaa na Shinyanga vijijini. 

Kusambaza shajala za kununulia zao la pamba : Katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa ununuzi wa zao la pamba SHIRECU ilifanikiwa kusambaza shajala katika vyama vya msingi (AMCOS) 121, na jumla ya shajala 2086 zilisambazwa zikiwa ni stakabadhi za fedha,hati za malipo na stakabadhi za mazao katika halmashauri za Shinyanga manispaa na Kishapu. 

Kutoa elimu kwa wakulima: SHIRECU kwa kupitia vyama vya msingi (AMCOS)116 imefanikiwa kutoa elimu kwa muda wa siku 5 kuhusu utaratibu wa kujiunga na AMCOS,wakulima wa AMCOS kufungua akaunti na kutunza takwimu sahihi za ununuzi wa pamba,jumla ya wakulima 116 walinufaika kutoka katika halmashauri za Kishapu, Manispaa na Shinyanga vijijini. 

Kuhamasisha vyama vya msingi (AMCOS) kufungua akaunti: Kwa ushirikiano wa Benki ya Posta na NMB,Menejimenti ya SHIRECU iliendesha mafunzo ya kuhamasisha AMCOS na wakulima kufungua akaunti katika vituo vya mafunzo vya Uzogore,Iselamagazi,Mhunze,Mwamashele,Bubinza,Lwagalalo na Mwamadulu.Pia ilihusisha mafunzo kwa makatibu katika uandishi wa vitabu na utunzaji wa kumbukumbu. Zoezi limekuwa endelevu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2019/2020. 

Katika kuendelea kuwahudumia wakulima kupitia vyama vya msingi SHIRECU imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ili huduma ziweze kuwafikia wakulima kwa urahisi. 

Imetolewa na: 

Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 
Shinyanga Regional Cooperative Union (SHIRECU(1984)LTD). 
25.02.2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527