WATUMISHI WA SERIKALI WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI MTONI WAAGWA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, February 25, 2019

WATUMISHI WA SERIKALI WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI MTONI WAAGWA

  Malunde       Monday, February 25, 2019Miili ya wataalam tisa wa idara ya ardhi na idara nyingine za Serikali waliofariki kwa ajali ya gari baada ya kutumbukia Mto Kikwawila , inaagwa leo Februari 25, katika viwanja vya Can, Tangani mjini Ifakara.

Kwenye tukio hilo Viongozi mbali mbali wa serikali wamehudhuria, akiwemo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe, pamoja na wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero na Ifakara.

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi ya Februari 23 saa 11 jioni katika Mto Kikwawila baada ya gari aina ya Toyota Land Cruiser Hard Top linalomilikiwa na wilaya ya Kilombero, kutumbukia kwenye mto huo na kusababisha vifo vya watumishi hao wa kitengo cha upimaji ardhi, huku wanne wakijeruhiwa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post